Message from Authors

We give valuable information to optimize and promote rational use of medicine in popular language. Information is a powerful tool that can benefit or harm the public, we bring you information to benefit and promote health. If you do not understand Swahili, highlight the content and translate to any language to get the intended message. Follow us, subscribe and ask any question for help. Karibu.

Thursday, 13 July 2017

NJIA ZA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA UTUMIAJI WA DAWA

Katika jamii yetu kumekuwa na mazoea katika utumiaji wa dawa, bila kuzingatia kuwa dawa yeyote isipotumika ipasavyo yaweza kuwa sumu na kuleta madhara makubwa kwa watumiaji. Kumekuwa na tabia ya kununua dawa hizo iwe katika hospitali au maduka ya dawa bila kuuliza au kupewa taarifa zinazoweza kusaidia utumiapo dawa hizo. Katika aya zifuatazo, tumeainisha taarifa gani ni za msingi kwako kama mtumiaji ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima yanayoweza kutokea utumiapo dawa:-



Ongea na daktari wako, mfamasia au mtaalamu wa afya kuhusu;
  • Kitu chochote ambacho kinaweza kuathiri uwezo wako wa kutumia dawa, kama vile shida ya kumeza au kukumbuka kumeza dawa.
  • Kuwaambia kama wewe ni au unatarajia kuwa na mimba, au kama wewe unanyonyesha mtoto.
  • Daima uliza maswali yako kwa wataalamu wa afya kuhusu matatizo yoyote au mawazo unaweza kuwa nayo.
  • Kuwaambia kama una allegy au hupata athari fulani kuhusu dawa husika (Allergy and sensitivity reactions). 
Jua dawa zako unazotumia.
  • Jina la dawa
  • Mwonekano wake
  • Jinsi ya kuhifadhi  vizuri
  • Wakati, jinsi, na kwa muda gani unapaswa kutumia dawa zako
  • Hali gani ukipata wakati wa kutumia dawa unapaswa kuwaona wataalamu wa afya.
  • Nini cha kufanya kama umeruka dozi yako (missing a dose)
  • Nini unatakiwa kufanya na baada ya muda gani utarajie matokeo
  • Madhara na mwingiliano kati ya vyakula, vinywaji au dawa na dawa unazotumia na namna ya kuepuka
  • Kama unahitaji vipimo vyovyote au ufuatiliaji (tests and monitoring)
  • Daima omba uandikiwe maelezo kuhusu dawa.
Soma “Label” na fuata maelekezo
  • Hakikisha unaelewa maelekezo, uliza kama una maswali au wasiwasi.
  • Daima hakikisha kama umepewa dawa sahihi.
  • Weka dawa katika chombo cha cha awali cha kuhifadhia, wakati wote iwezekanavyo.
  • Kamwe usichanganye madawa mbalimbali katika chupa moja.
  • Soma “label” na fuata maelekezo kutoka kwa mfamasia au daktari. Ukiacha dawa au unataka kutumia dawa tofauti kuliko ilivyoagizwa, shauriana na mtaalamu wa afya kwanza.
Kuepuka mwingiliano (avoid interactions)
  • Uliza kama kuna mwingiliano na madawa mengine yoyote au virutubisho malazi (ikiwa ni pamoja na vitamini au virutubisho mitishamba), vinywaji, au vyakula.
  • Kabla ya kuanza dawa yoyote mpya au kuongeza virutubisho (ikiwa ni pamoja na vitamini au virutubisho mitishamba), uliza tena kama kuna uwezekano wa mwingiliano na dawa unayotaka kuanza kutumia.

Kufuatilia Athari za dawa  yako '- Na Madhara ya Bidhaa nyingine unazotumia
  • Kuuliza kama kuna kitu unaweza kufanya ili kupunguza madhara, kama vile kula kabla ya kumeza dawa ili kupunguza mvurugano wa dawa au kunywa maji mengi mf. Ciprofloxacin  au kula aina fulani ya chakula mf. Chakula chenye mafuta katika kutumia dawa ya malaria ijulikanayo kama mseto (ALU).
  • Kuwa makini na namna unajisikia, kumbuka mabadiliko yoyote. Andika mabadiliko ili uweze kukumbuka kumweleza daktari wako au mfamasia.
  • Kujua nini cha kufanya kama ukipata madhara na wakati wa kumwaarifu daktari au mfamasia wako.
  • Kujua wakati gani unapata nafuu kutokana na utumiaji wa dawa hiyo/hizo.
 Kupata taarifa kutoka kwa mtaalam wa afya ni haki yako ya msingi na usiogope kuuliza maswali, na hakikisha unalidhika na kuelewa maelekezo utakayopewa.

No comments:

Post a Comment