Mungu kamuumba binadamu katika hatua kuu nne (4), kuzaliwa, kukua, kuzeeka na kufa. Katika hatua hizi, kuna vikwazo mbali mbali ambavyo binadamu hukutana navyo, na moja ya jambo nyeti sana ni afya. Wasomi mbali mbali wanamitazamo tofauti juu ya lini maisha ya binadamu huanza; wengine husema maisha huanza baada tu pale yai la mwanamke linapokutana na mbegu ya kiume (fertilization), wengine husema maisha huanza baada ya mbimba kukua na kufikisha umri wa miezi mitatu (first trimester) na wengine husema maisha ya binadamu huanza baada ya kuzaliwa. Yote ni mitazamo tu ambayo inaongozwa na itikadi na misimamo mbali mbali.
Mimba ni kati ya jambo linalopaswa kupewa kipaumbe sana kutokana na asili yake. Moja ya changamoto kubwa ambayo mwanamke mja mzito hukutana nayo ni upungufu wa kinga mwilini; hii husababishwa na mabadiliko ya kifiziolojia (physiologic changes) ili mwili uweze kuzoea na kulea mimba. Hali hii huhitaji umakini mkubwa sana ili kujikinga na magonjwa mbali mbali, moja wapo ni malaria, virusi na bakteria.
Moja kati ya vimelea hatari sana kwa maisha ya mtoto aliyetumboni ni bakteria ajulikanae kwa jina la Listeria monocytogenes, bakteria huyu ana sifa zilizo tofauti sana na bakteria walio wengi, na mbaya zaidi amesahaulika na kudharaulika sana katika sekta za afya, haswa katika matibbu na vipimo kwa wajawazito. Baadhi ya sifa zake zinazomfanya kuwa tofauti ni:
![]() |
Picha na themonitordaily.com. Bakteria Listeria monocytogenes |
- Sio rahisi kumkuza katika maabara (culturing), na hivyo kupelekea kushindwa kumtambua na kumchanganya na vimelea vingine visivyokuwa na madhara
- Anauwezo mkubwa wa kuishi na kuzaliana vyema katika baridi la -18͒ C, bakteria wengine hawawezi kukua katika baridi kali kiasi hicho, na hivyo ana uwezo wa kuambukiza kutoka katika vyakula vilivyotunzwa vyema katika friji na tayari kwa kuliwa.
Maradhi yatokanayo na bakteria huyu (Listeriosis) yanakadiliwa kuwa 30% kwa watu walio katika hatari; wanawake wajawazito, watoto wachanga na wazee. Na kwamba takribani vifo kati ya 400 na 500 hutokea kila mwaka, ni bakteria wa tatu kuongoza kuleta maradhi yatokanayo na kula chakula chenye kimelea huyu, (food poisoning).Wajawazito na watoto wachanga, wazee na watu waliopungukiwa kinga ya mwili wapo katika hatari kubwa zaidi ya kuugua ugonjwa huu (listeriosis).
Bakteria huyu huleta madhara yapi katika mwili?
Baadhi ya madhara yasababishwayo kimelea hiki ni:-
- Huathiri mfumo wa ubongo (mengitis au meningoencephalitis)
- Vidonda katika safu za macho (corneal ulcer)
- Mfumo wa upumuaji na kusababisha mgonjwa kupata shida ya kupumua (pneumonia)
- Kuathhiri mfuko wa uzazi na mlango wa uzazi, hali hii husababisha mimba haswa iliyo na umri wa miezi mitatu (3) hadi ishirini na nne (24) kutoka, mtoto kupoteza maisha kabla ya kuzaliwa au kuzaa kabla ya wakati (mtoto njiti)
Dalili za listeriosis ni zipi?
Kwa mwanamke mja mzito atapata dalili zifuatazo:-
- Joto la mwili kupanda na dalili za homa kama uchovu, maumivu ya kichwa
Maambukizi wakati wa ujauzito na kwa mtoto mchanga yanaweza leta madhara mbalimbali yakiwemo;-
- Wajawazito wapo katika hatari ya kupata Listeriosis mara kumi zaidi ya watu wengine
- Wajawazito wenye asili ya Kihispania wapo katika hatari ya kupa Listeriosis mara 24 zaidi ya watu wengine
- Mbaya zaidi, wajawazito wanauwezo wa kumuambukiza mtoto aliepo tumboni mwake
- Ugonjwa huu wa Listeriosis unaweza kusababisha kutoa kwa mimba, kuzaa mtoto akiwa ameshakufa, kuzaa mtoto kabla ya kufikisha umri wake/mtoto njiti (Preterm labor)
- Ugonjwa huu unaweza sababisha mtoto mchanga kupoteza maisha.
Kwa watu wengine (wasio na mimba), hupata dalili zifuatazo:-
- Kukakamaa kwa shingo
- Hali ya kuchanganyikiwa
- Kifafa/ukakamavu wa misuli
- Joto la mwili kupanga
- Maumivu ya misuli
- Kizunguzungu (loss of balance)
Ikumbukwe kuwa bakteria huyu huathiri zaidi wajawazito, watoto wachanga, wazee na watu waliopungukiwa na kinga ya mwili
Bakteria huyu anapatikana wapi?
Bakteria huyu hupatikana katika maeneo yafuatayo:-
4. Mazingira ya kutunza nyama na machinjioni kuwa safi muda wote
Ni basi, ni muhimu kuzingatia kuwa, kuhifadhi vyakula katika friji haikuepeshi na magonjwa yatokanayo na bakteria, na hivyo ni vyema kuzingatia kanuni za usafi na kuhakikisha kuwa tunakula vyakula salama kwa kulinda afya zetu, watoto, wajawazito na wazee.
Na ikumbukwe kuwa makala hii haiondoi sababu zingine zinazoweza kuleta matatizo tajwa, bakteria huyu ni moja tu ya chanzo cha matatizo hayo, hivyo ni muhimu kufika katika kituo cha afya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Bakteria huyu hupatikana katika maeneo yafuatayo:-
- Mimea mbali mbali mfano, mboga za majani na matunda
- Mifugo mfano ng'ombe na kondoo, pamoja na mazao yake kama vile maziwa na nyama
- Ndege
- Udongo
- Hakikisha unanawa mikono yako kwa sabuni kabla ya kula
- Hakikisha unaosha matunda kabla ya kula
- Hakikisha unaosha vyema mbogamboga kabla ya kuchemsha
4. Mazingira ya kutunza nyama na machinjioni kuwa safi muda wote
Ni basi, ni muhimu kuzingatia kuwa, kuhifadhi vyakula katika friji haikuepeshi na magonjwa yatokanayo na bakteria, na hivyo ni vyema kuzingatia kanuni za usafi na kuhakikisha kuwa tunakula vyakula salama kwa kulinda afya zetu, watoto, wajawazito na wazee.
Na ikumbukwe kuwa makala hii haiondoi sababu zingine zinazoweza kuleta matatizo tajwa, bakteria huyu ni moja tu ya chanzo cha matatizo hayo, hivyo ni muhimu kufika katika kituo cha afya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment