Message from Authors

We give valuable information to optimize and promote rational use of medicine in popular language. Information is a powerful tool that can benefit or harm the public, we bring you information to benefit and promote health. If you do not understand Swahili, highlight the content and translate to any language to get the intended message. Follow us, subscribe and ask any question for help. Karibu.

Monday, 31 July 2017

EPUKA VIPODOZI VYENYE VIAMBATA SUMU HIVI (DYING TO BE WHITE)

Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imekuwa ikifanya juhudi mbali mbali ili kulinda afya za watumiaji wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba vinavyotengenezwa au vinavyoingizwa nchini. Moja ya juhudi kubwa inayofanya kuwalinda watumiaji ni kuzuia uingizwaji wa vipodozi vyenye viambata sumu ambavyo vina madhara kwa watumiaji, na kuviondoa sokoni vipodozi vilivyoingizwa na wafanya biashara wasio waaminifu. 
Kumekuwa na upuuzwaji mkubwa sana hasa kwa akina dada na badhi ya wanaume wanaotumia vipodozi hivyo kubadilisha rangi ya miili yao (kujichubua) ili wavutie/ wapendeze. Vipodozi hivi vina viambata sumu ambavyo vina madhara makubwa sana kwa watumiaji wake, na ni jambo linalotakiwa kutiliwa mkazo.  
Baadhi ya madhara yatokanayo na vipodozi hivyo ni:-
  • Kansa ya ngozi, figo, ini; figo kushindwa kufanya kazi
  • Ugumba/utasa
  • Magonjwa ya ngozi mf. fangasi, chunusi; mabaka; muwasho/mzio au kidonda kutopona haraka iwapo ngozi itapata jeraha au kufanyiwa upasuaji
  • Kuumwa kichwa; kizunguzungu, uziwi; upofu na upotevu wa fahamu mara kwa mara.
  • Magonjwa ya moyo; mishipa ya fahamu
  • Mimba kuharibika au kusababisha madhara kwa mtoto tumboni mf.  kuharibu ubongo
  • Mwanamke kuota ndevu 
  • Madhara ya kiuchumi  baada ya mtumiaji kuathirika
Ni muhimu kuangalia viambata vilivyo ndani ya vipodozi kila mara ununuapo, ili kuhakikisha viambapa sumu vifuatavyo havipo katika kipodozi/vipodozi hivyo. Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, imepiga marufuku vipodozi vyote vilivyo na viambapa sumu vifuatavyo:-
  • Mercury
  • Vinyl Chloride
  • Chlorofluorocarbons
  • Zirconium
  • Steroids
  • Chloroform Propellants
  • Hydroquinone
  • Methyl Chloride
  • Bithionol
  • Halogenated Salicylanilides 
  • Hexachlorophene
    Ikumbukwe kuwa, hata kama unapakaa kwenye ngozi, viambata hivi vina uwezo wa kupenya kwenye ngozi na kuingia ndani ya mwili, na hivyo kuleta madhara kama yaliyotajwa hapo awali. Jari afya yako, epuka vipodozi hivyo kwa usalama wa maisha yako.

No comments:

Post a Comment