Message from Authors

We give valuable information to optimize and promote rational use of medicine in popular language. Information is a powerful tool that can benefit or harm the public, we bring you information to benefit and promote health. If you do not understand Swahili, highlight the content and translate to any language to get the intended message. Follow us, subscribe and ask any question for help. Karibu.

Tuesday, 11 July 2017

MTAMBUE MFAMASIA WAKO

Watu wengi katika jamii ya Tanzania, inamtambua mfamasia kama mtu yeyote anaetoa dawa. Mtazamo huu si sahihi hata kidogo. Mfamasia ni mtaalamu wa dawa ambae hutoa huduma mbali mbali za kiafya mfano, ushauri kuhusu matumizi sahihi ya dawa, kufanya tafiti katika taasisi mbalimbali katika maswala yanayo husu afya haswa pale ambapo dawa zinahusishwa moja kwa moja, kusimamia utengenezaji wa dawa viwandani, kusimamia utoaji wa huduma za afya katika maduka ya dawa, n.k. Ili ukidhi vigezo vya kuwa mfamasia Tanzania, unapaswa kusajiliwa na Baraza la Famasi Tanzania kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Famasi ya Mwaka 2011.
Mfamasia katika maabra ya kuhakiki ubora wa dawa
Katika Hospitali, Mfamasia huhakikisha dawa anayopewa mgonjwa ni sahihi na inamaelezo sahihi kwa ugonjwa. Kutoa maelezo ya kina juu ya dawa ni wajibu wa mfamasia.
Wafamasia wakikagua dawa na kuziandaa kabla ya kutoa huduma kwa wagonjwa.
Kwa Tanzania Taaluma hii ya Famasi ilianzishwa takribani miaka 43 iliyopita kukiwa na chuo kimoja tu cha Dar-es-Salaam, Ikiwa kama Idara ya Famasi (Pharmacy Department) chini ya kitivo cha utabibu (Faculty of Medicine). Hivi sasa Tanzania kuna vyuo takribani vinne (4) vinavyotoa taaluma hii. Ili uweze kukidhi vigezo vya kusoma shahada ya famasi mwanafunzi anapaswa awe na ufaulu mzuri katika masomo ya Physics, Chemistry and Biology, ambayo ndo haswa kitovu cha taaluma hii.

Chini ya mfamasia kuna taaluma mbali mbali za dawa mfano Diploma in Pharmaceutical sciences, Certificate in Pharmaceutical Sciences. Na hivi karibuni Baraza la Famasi limeanzisha course fupi mbili ambazo zinajulikana kama ADDO (Accredited drug dispensing outlet) dispensers na Medicine dispensers, ili kukabidiliana na upungufu wa wataalamu wa dawa vijijini (kwa maelezo zaidi tembelea http://pc.go.tz/addo). Mfamasia husimamia wanataaluma wote hawa ili kutoa huduma sahihi ya dawa kwa wagonjwa.
Hivyo basi ni wajibu wako na ni muhimu kujua kuwa, kila mara utembeleapo katika duka la dawa lilipo mtaani, jilidhishe kuwa lina vibali halisi kutoka mamlaka husika na pia uulize taarifa mbali mbali kuhusu dawa unayopewa mfano, madhara ya kutalajia (side effects) pindi unapotumia dawa hiyo/hizo, vitu gani vya kuepuka kufanya pindi unatumia dawa hizo, na pia jilidhishe kuwa dawa hiyo haijaisha muda wake wa matumizi. Ni muhimu na ni hakiyako ya msingi, pale inapohitajika omba ukutane na mfamasia.
Hivyo ni muhimu kumtumia mfamasia ili kuepuka madhara yatokanayo na dawa.

No comments:

Post a Comment