1.0 UTANGULIZI
Kwa watu wengi, matumizi ya dawa ni sehemu ya kawaida ya mara kwa mara ya maisha yao ya kila siku, na madawa haya hutegemewa kutibu ugonjwa na kuboresha afya. Ingawa dawa zinaweza kufanya wewe kujisikia vizuri na kukusaidia kupata afya njema, ni muhimu kujua kwamba madawa yote yana athari pamoja na faida zake.
Faida za dawa ni pamoja na kupunguza shinikizo la damu, kuponya maambukizi na kutuliza maumivu. Athari za dawa ni pamoja na vidonda vya tumbo au athari kubwa zaidi kama uharibifu wa ini na figo.
2.0 DAWA NI NINI?
Dawa hutumika kuuasaidia mwili dhidi ya magonjwa (kinga na kutibu), kuondoa dalili za magonjwa, kutibu majeraha na maumivu n.k.

3.0 MATUMIZI SAHIHI YA DAWA NI NINI?
· Ni kutumia dawa kulingana na utambuzi wa kitabibu (medical diagnosis/clinical needs) au ugonjwa husika.
· Kutumia dawa kwa muda unaotakiwa kama ulivyoelekezwa na wataalamu wa dawa.
· Kutumia kiasi sahihi cha dawa kama ulivyoelekezwa.
· Kutumia dawa sahihi (proper medicine).
· Kutumia dawa kwa usahihi (proper dose interval).
4.0 MATUMIZI YASIYO SAHIHI YA DAWA NI PAMOJA NA;
· Matumizi ya dawa nyingi kwa mgonjwa (Polypharmacy)
· Matumizi ya dawa za sindano wakati dawa za kumeza zingefaa zaidi
· Kutumia dawa chini au zaidi ya dozi iliyoelekezwa.
· Maamuzi ya kujitibu mwenyewe na tena kwa dawa isiyosahihi (self medication)
· Kutumia dawa bila kufuata maelekezo ya mfamasia au daktari
· Kutomaliza doseji ya dawa.
5.0 SABABU ZINAZOSABABISHA MATUMIZI YASIYO SAHIHI YA DAWA
· Imani potofu juu ya dawa fulani/ mazoea
· Mategemeo/mahitaji ya mgonjwa (demand/expectation from patient)
· Kuwepo na taarifa isiyo sahihi
· Ukosefu wa elimu juu ya athari za dawa
· Mzigo mgonjwa(patient load lead to poor Rx)
· Ukosefu wa wataalamu wa afya wa kutosha
· Ukosefu wa mawasiliano kati ya wataalamu wa afya na wagonjwa.
· Ukosefu wa vifaa vya uchunguzi; husababisha ugumu katika kutambua ugonjwa hivyo husababisha daktari kumwandikia mgonjwa dawa nyingi (lack of diagnostic facilities---promotes polypharmacy)
6.0 AINA ZA ATHARI KUTOKANA NA MATUMIZI YA DAWA.
Kuna aina kadhaa za athari kutokana na matumizi ya dawa
- Uwezekano wa mwingiliano hatari kati ya dawa, chakula na vinywaji. Mchanganyiko wa vitu hivi inaweza kuongeza nafasi ya kuwa kunaweza kuwa na mwingiliano.
- Uwezekano wa kwamba dawa inaweza isifanye kazi kama ilivyotarajiwa.
- Uwezekano kwamba dawa inaweza kusababisha matatizo ya ziada.
7.0 FAIDA ZA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA
· Hupunguza uwezekanao wa kujenga usugu kwa vimelea kama malaria, virusi, fangasi na bacteria.
· Hupunguza madhara ya dawa.
· Kupunguza gharama za matibabu.
· Hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yatokanayo na utumiaji sugu wa dawa.
· Huboresha afya ya mtumiaji wa dawa.
8.0 HASARA ZITOKANAZO NA MATUMIZI MABAYA YA DAWA
· Kujenga usugu wa vimelea mf. malaria, virusi, fangasi na bakteria dhidi ya dawa (drug resistance).
· Husababisha magonjwa kama ugonjwa wa figo, Ini n.k.
· Husababisha usugu wa ugonjwa (Chronicity).
· Kuongeza madhara ya dawa( in case of overdose/over use or short dose interval than directed).
· Upotevu wa pesa pamoja na mali- kuongeza gharama za matibabu
· Kusababisha ulemavu (mtu mzima/kichanga)
· Kupoteza maisha
9.0 MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA KUTOKANA NA MATUMIZI MABAYA YA DAWA (KUTOTUMIA DAWA KWA USAHIHI)
Watu wengi wamefanya dawa kuwa kama chakula au pipi! Jambo ambalo linasikitisha sana, kati ya vitu ambavyo si vyema sana kuzoea kutumia ni dawa maana dawa si rafiki wa mwili pale isipotumika ipasavyo, dawa ni sumu.
Kuna madhara mbalimbali mabli yanoyoweza kujitokeza dawa isipotumika ipasavyo, na baadhi ya madhara nimeyaongelea hapo awali. Madhara haya yanaweza kuwa ya yale yanayotokea baada ya muda mfupi au ya muda mrefu.
Madhara yanayotokea baada ya muda mfupi ni rahisi sana kuyatambua. Madhara yanayotokea baada ya muda mrefu si rahisi kuyatambua, madhara haya hutokea baada ya miaka kadhaa baad ya kutumia baada ya muda mrefu, na utapata madhara haya katika hatua fulani ya maisha yako na haitakuwa rahisi kutambua kama yamesababishwa na dawa maana pia madhara hayo hayategemei kitu kioja ili kutokea baali yanahitaji pia mambo kadhaa wa kadhaa ili yatokee.
Baadhi ya dawa zinazotumika isivyopaswa mara kwa mara katika jamii zetu ni pamoja na dawa za dawa za kutibu magonjwa yatokanayo na bacteria lakini pia kuna wimbi kubwa la ongezeko la matumizi mabaya ya dawa za kuongeza nguvu za kiume kwa vijana katika jamii zetu.
I.
No comments:
Post a Comment